Vodacom Tanzania inayo furaha kutangaza kuunganishwa kwa My Vodacom App na M-Pesa Supa App, hatua inayolenga kurahisisha na kuboresha zaidi huduma kwa wateja.
Kupitia muunganiko huu, wateja wataweza kufurahia huduma zote wanazozipenda za Vodacom kwenye aplikesheni moja, hivyo kuongeza ufanisi na urahisi wa matumizi.
Kama sehemu ya mabadiliko haya, My Vodacom App itasitishwa rasmi tarehe 1 Desemba 2024. Tunawahimiza wateja wote kupakua na ku-update M-Pesa Supa App ili kuendelea kufurahia huduma zetu bila usumbufu.
Hatua hii inadhihirisha dhamira yetu ya kuboresha huduma kwa wateja kupitia suluhisho za kibunifu.
Asante kwa kuichagua Vodacom Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...