Na.Ashura Mohamed – Arusha.

Tanzania imeandika historia kubwa baada ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Science kushinda tuzo nne za heshima katika mashindano ya kimataifa ya Ufanisi kwa Vijana (Junior Achievement) yaliyofanyika nchini Mauritius yakihusisha mataifa 11 kutoka barani Afrika.

Wanafunzi hao wa Kidato cha Sita kutka shule ya Arusha Science  kupitia kampuni yao ya BLOOMTECH wameweza  kubuni programu inayosaidia wakulima kupata suluhisho la changamoto mbalimbali zinazokabili mazao yao.

Aidha  Ubunifu huo umeliwezesha Tanzania kushinda Tuzo ya Umahiri wa Ujasiriamali Tuzo ya Matumizi Bora ya Usimamizi wa Miradi

Tuzo ya Uongozi wa Wasichana (Girl LEAD Award)Tuzo Kuu – Mshindi wa Kwanza.

Wanafunzi hao  waliowakilisha Tanzania,ni pamoja  na  Yvonne Lyaruu,Baraka Kileo na Angel Mtakwa, walionyesha uongozi wa kipekee na ushindani wa hali ya juu, wakitangaza ushindi huo kuwa si wao tu bali ni wa taifa zima.

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari  Arusha  Science, Prof. Nuhu Hatibu amesema matokeo haya yametokana na utekelezaji wa sera ya taifa ya elimu ya amali, ambapo amehimiza serikali kuwekeza zaidi katika eneo hili.

Amesema shule hiyo ya Arusha Science  wamejikita  katika kuhakikisha elimu ya vitendo inatekelezwa kikamilifu huku ushindi huo ni uthibitisho wa uwezo wa Tanzania kushindana kimataifa.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Yvonne amesema kuwa walipata  changamoto kubwa kwa sababu washiriki wote walikuwa wamejiandaa vizuri lakini, waliongeza kujiamini kuwa wanaweza kushinda na wamefanikiwa kwa Juhudi zao na imani thabiti.

Kwa Upande wake Baraka Kileo ameongeza Mashindano haya yalihusisha nchi 11 za Afrika, na kupitia kampuni yao ya BLOOMTECH, tumeibuka kuwa kampuni ya mwaka barani Afrika.

Angel Mtakwa amesema kuwa ushindi huo pia umeonyesha uwezo wa wasichana kwenye uongozi, hasa baada ya kushinda Tuzo ya Girl LEAD Award, ambayo imewapa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania nchini Ghana mwaka 2025.

Nae Mratibu wa mashindano kutoka taasisi ya The Foundation for Tomorrow, aliyeambatana na wanafunzi hao, Harun Kidungu,alisema:

Mashindano hayo yanalenga kuwasaidia vijana kujitegemea kupitia ubunifu ambapo suluhisho walilobuni linaonyesha njia mpya ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, ambalo ni changamoto kubwa duniani.

Baadhi ya wazazi akiwemo Dororosa Dankani,Mzazi wa mmoja wa wanafunzi, aliwataka wazazi wenzake kuwaruhusu watoto wao kutumia vipaji vyao badala ya kuwalazimisha masomo yasiyoendana nao.

"Ndugu zangu wazazi kwa mfano huu  ni dhahiri kuwa talanta za watoto wetu zinaweza kuwafanikisha zaidi nawaomba hebu tuwaunge mkono," alisema Dororosa.

Ushindi wa wanafunzi wa Arusha Science sio tu umeitangaza Tanzania, bali pia umeyapiku mataifa makubwa kama Afrika Kusini,Nigeria, na Kenya na BLOOMTECH sasa inaandaa mikakati ya kushiriki mashindano ya kidunia nchini Brazili mwaka 2025, hatua ambayo inazidi kuiweka Tanzania katika ramani ya ubunifu wa kimataifa.

Wanafunzi waliofanya Vizuri wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa  wa KIA,Mara baada ya kuwasili nchini


Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Arusha Science Prof Nuhu Hatibu akiwa ameshilikilia Kombe la Ushindi la Wanafunzi kutoka Shule yake


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...