Na Oscar Assenga,TANGA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Ndugu Msafiri Mbibo amesema wizara hiyo inatambua mchango wa wanajiosayansi katika Vision 2030 hivyo itaendelea kuwatuma kikamilifu ili kuwawezesha utekelezaji wa ndana hiyo.

Mbibo aliyasema hayo Desemba 4,2024 Jijini Tanga wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Wanajiosayansi kwa niaba ya Waziri wa Madini ambapo alisema wanajiosayansi ni nguzo muhimu katika kufanikisha dhana ya Vision 2030.

Alisema kwamba wataendelea kufanya hivyo kutokana na kwamba wanajiosayansi ni nguzo muhimu katika kufanikisha dhana ya Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri.

Aidha alisema katika kufanikisha Vision 2030,wanajiosayansi wameendelea kutumia utaalamu wao katika kufanya utafiti wa kina wa kijiofizikia kwa kutumia teknolojia za kisasa kwa lengo la kutambua tabia za miamba.



Alisema Utambuzi huo utawezesha kufanyika kwa tafiti nyingine za jiosayansi zenye kuwezesha kubaini aina mbalimbali za madini yapatikanayo nchini .


Mbibo aliwashukuru wanajiosayansi kwa utayari wao wa kubeba maono ya Vision 2030 na kutoa msaada wa kitaalamu katika kufikia utekelezaji wake.


Kupitia dhana ya Vision 2030, Wizara ya Madini inalenga kufanya tafiti za kina kwa angalau asilimia 50 kufikia asilimia 2030, ukilinganisha na sasa ambako ni asilimia 16 pekee ndiyo imefanyiwa utafiti wa kina kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Awali akizungumza, Rais wa Jumuiya ya Wanajiolojia Tanzania, Dkt. Elisante Mshiu, alisema kuwa mkutano huo unalenga kujadili mabadiliko katika sekta ya nishati, ikiwa ni pamoja na mpito kutoka kwa nishati chafuzi kwenda kwenye nishati salama, ambayo ni sehemu ya malengo ya serikali.



Dkt. Mshiu alisisitiza kuwa bila kuwa na Bodi ya Usajili ya Wanajiosayansi, maono ya 2030 yanaweza kukutana na changamoto kubwa. Alitoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa juhudi za uundwaji wa bodi hiyo zinafanyika kwa haraka ili kuendana na kasi ya maendeleo ya nchi.

"Kupitia Wizara ya Madini, juhudi kubwa zinafanyika na hatua hizo ziko karibu kumalizika. Tumesisitiza umuhimu wa kuharakisha mchakato huu ili kuhakikisha maendeleo yanakua kwa kasi inayohitajika," alisisitiza Rais Mshiu.



Wanajiosayansi kutoka ndani na nje ya Tanzania walikusanyika jijini Tanga kwa mkutano wa TGS 2024, ambao unalenga kupeana taarifa za kitaalamu, kubadilishana uzoefu, na kujadili masuala yanayohusu utafutaji na uendeshaji wa rasilimali za madini, mafuta, gesi asilia, maji, na joto la ardhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...