Na; Mwandishi Wetu - DODOMA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imeendelea kufanya maboresho zaidi katika matumizi ya TEHAMA ili kutoa huduma kwa urahisi kwa wanachama wake na wastaafu.

Mhe.Katambi ameyasema hayo hii leo Januari 31, 2025 Bungeni, jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Tecla Ungele ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka huduma za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika ngazi za wilaya na tarafa ili kuwaondolea usumbufu wastaafu kwenda kuhakiki mkoani.

Akijibu swali hilo, Mhe. Patrobas Katambi amesema Wastaafu kwa sasa wanaweza kujihakiki kupitia simu janja (Smartphone) kupitia programu ya kidijitali (Online Portal) bila kufika katika ofisi za Mifuko.

Ameongeza kuwa, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeendelea na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanachama, wastaafu na wadau wote wanao husika katika mtiririko wa mafao kuhusu huduma zinazotolewa kupitia TEHAMA.

Kadhalika, Katambi amesema uhakiki wa uanachama unafanyika katika ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii zilizoko mikoani na wilayani na ukusanyaji wa taarifa ni shirikishi ngazi zote ikiwemo ngazi ya Tarafa, Wilaya na Mkoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...