Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia, Masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis L. Londo (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Kilimo, Maji, Mazingira na Maendeleo Vijijini na Mawaziri wa Mambo ya Nje uliofanyika jijini Kampala, Uganda. tarehe 10 Januari, 2025

Mkutano huo wa awali ambao ulikutanisha Mawaziri na Wakuu wa Taasisi Mbalimbali za Kimataifa kutoka barani Afrika umefanyika kabla ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Mpango Madhubuti wa Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP).

Mkutano huo umejadili masuala anuai juu ya upitishaii wa Azimio la Kampala kuhusu Mifumo Madhubuti na Endelevu ya Kilimo na Chakula barani Afrika (Kampala CAADP Declaration on Building Resilient and Sustainable Agrifood Systems in Afrika) ambalo madhumuni yake ni kubadili mfumo wa awali uliojikita kwenye kilimo pekee na kwenda kwenye Mifumo ya Kilimo Chakula (Agrifood).

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri wengine wa Sekta Mbalimbali ikiwemo Mhe. Hussein M. Bashe (Mb.); Waziri wa Kilimo, Mhe. Juma H. Aweso (Mb.), Waziri wa Maji, Mhe. Shamata S. Khamis (Mb.), Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar na Mhe. Alexander P. Mnyeti (Mb.) Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...