Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Mikataba ya wazabuni watakao zalisha chanjo kwajili ya kampeni ya chanjo kwa mifugo nchini iliyofanyika 21 Januari, 2025 jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu; Dodoma

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amewataka wazabuni waliopewa jukumu la kusambaza chanjo kwa ajili ya kampeni ya chanjo ya mifugo nchini kuhakikisha kazi hiyo wanaifanya vyema kwa kushirikiana na wazalishaji.

Ameyasema hayo wakati wa Hafla Fupi ya Utiaji Saini Mikataba baina ya Wizara na Wazabuni hao watakaosambaza Chanjo ya Mifugo Nchini iliyofanyika jijini Dodoma Januari 21, 2025.

Prof. Shemdoe ameongeza kuwa utoaji wa chanjo hiyo kwa mifugo inatakaiwa kufanyika chini ya uangalizi wa wazalishaji kwa kushirikiana na wataalamu watakao kuwa wanafanya kazi hiyo ili kusaidia kutatua changamoto zitakazojitokeza wakati wa zoezi hilo.

Aidha Prof. Shemdoe ametoa shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kuwezesha utowaji wa chanjo hiyo mwaka huu na kuwapa kipaumbele makampuni yanayozalisha chanjo ndani ya nchi kuweza kusambaza chanjo hiyo nchi nzima.

Kampuni zitakazotumika katika uzalishaji wa chanjo wa chanjo hiyo ni pamoja na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Hester Biosciences Afica Limited (HBAL) na Novel Vaccine and Biological Limited (NOVABI) l.

katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Mikataba ya wazabuni watakao zalisha chanjo kwajili ya kampeni ya chanjo kwa mifugo nchini iliyofanyika 21 Januari, 2025 jijini Dodoma.

Baadhi ya Wawakilishi wa Makamuni pamoja na wa Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walioshiriki katika zoezi la utiaji saini wa mikataba ya wazabuni watakaozalisha chanjo itakayotumika kwajili ya kampeni ya chanjo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...