Na Mwandishi Wetu,Ruvuma

CHAMA cha Mapinduzi wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,kimempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh.bilioni 145.77 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho Mwinyi Msolomi,wakati wa ziara yawajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Songea mjini baada ya kutembelea mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa na Mkandarasi kampuni ya China Civil Engineering Contruction Corporation(CCECC).

Mradi huo,unatarajiwa kumaliza kero ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea hasa wanaoishi mtaa wa Sokoine kata ya Bombambili na Making’inda kata ya Msamala ambao mara kwa mara wanapata maji kwa mgao.

Msolomi,ameishukuru Serikali kupitia wizara ya maji na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea(Souwasa), kuanza kutekeleza mradi huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Manispaa hiyo na maeneo mengine ya jirani.

Alisema,mradi huo ni muhimu kwani utakuwa suluhisho la changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji na utatoa fursa kwa wananchi wa Songea kupata muda mwingi kujikita katika shughuli zao za kiuchumi badala ya kutumia kwenda kutafuta maji.

Katibu wa Chama hicho wilaya ya Songea mjini James Mgego,ameiomba Serikali kuhakikisha inatoa fedha zilizobaki ili mkandarasi aweze kuendelea na utekelezaji wa mradi huo ambao umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.

“Tumekagua mradi huu na kulidhishwa na ubora wake,hata hivyo changamoto tuliyoelezwa na wataalam ni ukosefu wa fedha ambazo zingemwezesha Mkandarasi kuendelea na kazi ya ujenzi,sisi kama Chama kilichopewa dhamana na Watanzania tunaishauri Serikali itoe fedha kwa wakati ili mradi huu ukamilike kwa wakati kama yalivyo matarajio ya wananchi wa Manispaa ya Songea”alisema Mgego.

Alisema,kwa sasa wananchi wa Songea wanapata huduma ya maji lakini bado hayatoshelezi hasa kwenye kata za pembezoni,kwa hiyo mategemeo yao ni mradi huo ambao ukikamilika utatoa huduma ya maji kwa zaidi ya maiaka 20.

Naye Mjumbe wa kamati hiyo Pascal Msigwa,amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo,lakini ameiomba Serikali kuharakikisha ujenzi wake ili wananchi waweze kupata huduma ya maji ya uhakika na kuwaondolea adha ya kupata huduma hiyo kwa mgao.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Songea mjini(Souwasa) Vicenti Bahemana alisema,mradi ulianza kutekelezwa mwezi Januari 2024 na unatarajia kukamilika mwezi Septemba 2026.


Alisema,tayari Serikali kupitia wizara ya maji imeshamlipa mkanadarasi fedha za malipo ya awali kiasi cha Sh.bilioni 21.87 kati ya Sh.bilioni 145.77 ambayo ni gharama halisi ya utekelezaji wa mradi huo.

Alitaja kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa kidaka maji katika Mto Njuga chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 17 kwa siku,ujenzi wa mtambo wa kuchuja na kutibu maji lita milioni 16 na kujenga matenki matatu yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 9.

Kwa mujibu wa Bahemana, kazi nyingine zinazotekelezwa ni kulaza bomba za kusambaza maji urefu wa kilometa 30.2,upanuzi wa mtandao wa bomba za usambazaji maji kilometa 34.7 kukarabati mtambo wa kuchuja na kutibu maji lita milioni 11.5 ambao kwa sasa ufanisi wake upo chini ya kiwango ili kukidhi mahitaji.

“mpaka sasa mkandarasi amekamilisha ujenzi wa matenki mawili kati ya matatu yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 2 kila moja ambayo ni tenki la Chandamali na Milaya na tenki la Mahilo litakalo kuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 5 lipo katika hatua za uchimbaji wa msingi”alisema.

Alisema,mpaka kufikia tarehe 30 Novemba mwaka jana utekelezaji wa mradi umefikia asilimia zaidi ya 4.8 na utakuwa na mafanikio makubwa katika kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Songea.
 

Msimamizi wa mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa gharama ya Sh.bilioni 145.77 Mhandisi Vicent Bahemana,akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi  wilaya ya Songea mjini, kuhusu maendelea ya ujenzi wa mradi huo baada ya wajumbe hao kufika eneo la Mahiro ambako kunatarajia kujengwa tenki kubwa la kuhifadhi lita milioni 5 za maji.
 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea mjini  mkoani Ruvuma Mwinyi Msolomi katikati na katibu wa Chama hicho James Mgego kushoto, wakikagua tenki la  kuhifadhi maji lita milioni 2 eneo la Chandamali linalojengwa kupitia mradi wa maji wa miji 28 katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,kulia msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Songea(Souwasa) Mhandisi Vicent Bahemana.

 

Msimamizi wa mradi wa maji wa miji 28  kutoka Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea(Souwasa)Mhandisi Vicent Bahemana kulia,akionyesha mchoro wa mradi huo kwa wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mwinyi Msolomi aliyevaa kaunda suti wakati wa ziara ya wajumbe hao walipotembelea mradi huo jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...