Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo, ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Akiwa hapo, aliipongeza TCAA kwa usimamizi thabiti wa sekta ya usafiri wa anga na alipata maelezo kuhusu utendaji wa Mamlaka pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Maonesho haya yaenga kuonyesha mafanikio ya Zanzibar katika sekta mbalimbali tangu Mapinduzi ya mwaka 1964, na yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wananchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo, akiwa katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)



Timu ya maonesho ya TCAA ikiendelea kuwahudumia na kutoa elimu kuhusu fursa mbalimbali katika sekta ya usafiri wa anga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...