NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

MCHEZAJI wa ngumi za kulipa nchini Amiri Matumla ambaye ni mtoto wa Bondia Mstaafu; Rashidi Matumla amejitapa kumchapa mpinzani wake Pauls Amavila raia wa Namibia katika pambano litakalopigwa leo Februari 28,2025 katika ukumbi wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana wakati wa utambulisho wa mabondia watakaozichapa katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Mafia Boxing Promotion, Matumla amewataka mashabiki wake waweze kuhudhulia pambano hilo kwani anaamini ataibuka mshindi na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

"Mpinzani wangu ajipange, maana naenda kumpiga na kuweza kuondoka na ushindi hapo kesho, na ninamuahidi kama atafika raundi ya nane, nusu ya malipo yangu nitamkabidhi maana najua hawezi kufika mpaka raundi ya nane nitakuwa nimeshamkarisha". Amesema Matumla

Mkurugenzi wa Mafia Promotion, Ally Zayumba, akizungumza baada ya tukio hilo, amesema kutakuwa na mapambano 14 kwa mabondia wa ndani na nje ya nchi kuoneshana ubabe.

Mchakato wa kutambulisha mabondia hao lililokwenda sanjari na tambo kutoka kwa mabondia ilisababisha bondia Abdallah Pazzy 'Dullah Mbabe' almanusura azichape kavukavu na mpinzani wake.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila anatarajia kuwaongoza Watanzania kushuhudia mapambano hayo ya ngumi yasiyokuwa ya kuwania mkanda huku viongozi wengine wa Serikalini wanatarajiwa kuwepo.

Pamoja na hayo Kampuni ya Mafia Boxing Promotion imekabidhi majiko zaidi ya 30 ya gesi ya kupikia kwa mama lishe wa soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...