
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoenda sambamba na harambee ya uchangishaji wa fedha na vitu vingine, kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi. Jumla ya kiasi cha fedha takriban shilingi bilioni 1.7 zilipatikana. Hafla hiyo iliyowahusisha viongozi, wanachama, wafuasi wa CCM na wananchi wa kada mbalimbali, ilifanyika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo, jijini Dodoma, tarehe 9 Februari 2025.











Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...