Na. Benny Mwaipaja
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkuu wa Ushirikiano ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Mpana na Fedha Mashariki na Kusini mwa
Afrika (Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and
Southern Africa- MEFMI), Dkt. Louis Kasekende, ambapo pamoja na mambo
mengine, wamejadiliana namna Taasisi hiyo inavyoweza kuandaa mafunzo
maalumu katika nyanja za kiuchumi, Akili Mnemba (Artificial
Intelligence), na uchumi wa kijani ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalam
waliobobea katika nyanja hizo ili kuisaidia nchi kupata suluhisho la
mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea duniani kutokana na kasi ya ukuaji wa
teknolojia na mabadiliko ya sera za misaada na mikopo kutoka nchi
zinazoendelea.
Kikao
hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu-Hazina,
Jijini Dodoma, kimemshirikisha pia Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.
Emmanuel Tutuba, Baadhi ya Menejeimenti ya Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya
Tanzania, pamoja na MEFMI.
Macroeconomic
and Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa
(MEFMI), ni Taasisi ya Kikanda inayojihusisha na utoaji mafunzo kwa nchi
wanachama wake katika kuwajengea uwezo wa uendeshaji wa program za
maendeleo, katika usimamizi wa Uchumi Mpana na Usimamizi wa Fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...