Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewatoa hofu vijana ambao wanataka kuwania nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kuwa wakae tayari kuwani nafasi hizo kwakuwa ajenda ya Mitano Tena ni kwa Mgombea wa Urais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea wa Urais Mteule wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.


Ndg. Kawaida amesema hayo leo tarehe 17 Februari, 2025 wakati akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Chuo cha UVCCM cha Tunguu alipoenda kuweka jiwe la msingi.


"kumezuka tabia kwa Wawakilishi, Wabunge, ajenda ya mitano tena ilikuwa ya wawili tu Mwenyekiti wetu wa CCM na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar. Wasiwatishe vijana kuwa wao mitano tena, vijana nendeni mkagombee," amesisitiza Ndg. Kawaida



#UngujayaCCM

#KijananaKijani

#TunazimaZoteTunawashaKijani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...