Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, leo ametembelea Chuo Kikuu cha Dodoma, na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo.

Mhe. Stergomena alipokelewa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka, aliyeambatana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Bi. Suzan P. Mlawi, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma Prof. Razack Lokina na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Winester Anderson.

Mhe. Stergomena Tax amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Menejimenti ya Chuo katika kusimamia ubora wa taaluma, kutunza taswira ya chuo na kuweka msisitizo wa kuendelea kutatua changamoto zote kwa wakati, husani zile zinazohusiana na maendeleo ya wanafunzi.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, akimkaribisha Mkuu wa Chuo, amemwelezea mikakati ya namna Menejimenti ilivyojipanga kuendelea kusimamia ubora wa taaluma inayotolewa na Chuo, pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa masuala ambayo yanahitaji ufafanuzi kwa jamii.

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, akisaini kitabu cha wageni, ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Jengo la Benjamin Mkapa, Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Bi. Suzan P. Mlawi (wa kwanza kushoto) wakizungumza jambo na Mkuu wa Chuo na viongozi wajuu wa Chuo kikuu cha Dodoma wakati wa ziara iliyofanyika jengo la Benjamin Mkapa Dodoma.

Mkuu wa Chuo akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo wakiwa kwenye Mkutano na Mkuu wa Chuo alipofanya ziara leo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Winester Anderson, akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo.

Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka (wa kwanza kulia) akiwa na  Prof. Razack Lokina( wa kwanza kushoto), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma; wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo alipotembelea Utawala Mkuu leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...