Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Msama Promotions Alex Msama ametoa onyo kwa waimbaji wote wa nyimbo za Injili ambao wamekuwa wakishiriki katika majukwaa na wasanii muziki wa kidunia kwa kuwa kufanya hivyo ni kushiriki katika kumtukuza shetani.

Msama ambaye ni mdau mkubwa wa Muziki wa Injili ametoa onyo hilo hivi karibuni alipokea tuzo ya heshima ya kuwa muandaaji bora wa matamasha ya injili nchini Tanzania ambayo maarufu yalikuwa yanafahamika kwa jina la TAMASHA LA PASAKA

Amesema sio vizuri wanamuziki wa nyimbo za Injili kushiriki katika majukwaa ya muziki wa kidunia ambao kwa sehemu kubwa ni wa kumtukuza shetani.

“Nawaonya waache kushiriki madhabahu za shetani,2 Wakorinto 6: 14-18 Msiambatane pamoja na watu wasioamini, pia wajihadhari na kupenda pesa kwani pesa nyingine ni za maagano ya kuzimu” Alex MSAma

Aidha amewataka wanamuziki wa nyimbo zainjili kuacha tamaa ya fedha ambayo imekuwa ikisababisha wasanii hao kwenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki wa kidunia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...