Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Ndege Mkoani Dodoma akiwa amebeba Tuzo Maalum ya Kimataifa ya "The Global Goalkeeper Award" aliyokabidhiwa leo February 04, 2025 na Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita Zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais Samia amesema tuzo hiyo ni zawadi kwa Watoa huduma wote wa Sekta ya Afya ambapo amewapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya katika kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto.

Itakumbukwa kuwa Rais Samia ndio Rais wa Kwanza Barani Afrika kupata tuzo hiyo ya Kimataifa.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...