Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akifafanua jambo, kwa Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mha. Karim Ally, wakati Mha. Karim, alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwa Mkuu wa Mkoa 13.2.2025

......

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameitaka EWURA, kurahisisha zaidi utaratibu wa kupata leseni za kufanya biashara ya mafuta ya petroli, kwani wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe, wameamka na wako tayari kuwekeza katika biashara hiyo.

Aliyasema hayo leo, Tarehe 13.02.2025, wakati alipotembelewa na Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mha. Karim Ally kwa lengo la kuzungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya kanda.

“EWURA mnafanya kazi nzuri sana, uwekezaji katika sekta ya mafuta umeongezeka, niwaombe mrahisishe zaidi taratibu za kupata leseni za biashara hii, ikiwezekana taarifa muhimu na mrejesho ziwafikie hata kwa njia ya simu ili utekelezaji wa masharti ya leseni uwe rahisi” alisema.

Mhe. Mtaka, aliongeza na kusema, “pamoja na nishati ya mafuta pia dunia inaelekea kutumia magari ya umeme, hivyo itakua vizuri kama EWURA itaandaa mapema mazingira rafiki katika uwekezaji wa nishati katika magari nchini”

Awali akielezea kazi na majukumu ya EWURA, Mha. Ally alisema, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha EWURA, lengo kuu la udhibiti katika sekta ya petroli ni kulinda maslahi ya walaji, wauzaji wa bidhaa hiyo na Serikali, ambapo kwa pamoja ni wadau wakuu wa EWURA.



Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akifafanua jambo, kwa Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mha. Karim Ally, wakati Mha. Karim, alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwa Mkuu wa Mkoa 13.2.2025

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...