Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Unguja na Pemba zajengewa uwezo juu ya Namna ya Utayarishaji wa Bajeti zenye Vipaumbele vya Kijinsia katika Ukumbi wa ZMA Malindi.

Akifungua Mafunzo hayo Afisa Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara hiyo Zahra Nassor Said amesema lengo la kikao hicho ni kuwa andaa watendaji wa Wizara hasa wanaotayarisha Bajeti za Mashirika na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi katika Eneo la Utayarishaji Bora wa Bajeti, MTEF, PBB pamoja na Bajeti yenye kuzingatia masuala ya Usawa wa Kijinsia ili waweze kuendana na hali halisi ya Mipango mikuu ya Serikali.

Zahra amewataka Watumishi hao kuwa Watulivu na Wasikivu kwani Bajeti yoyote Itakayoandaliwa na Mashirika na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kama hazikuzibgatia mahitaji yaliyoainishwa na Wizara ya Fedha kupitia Tume ya Mipango na Kitengo cha Bajeti cha Wizara ya Fedha na Mipango basi bajeti hiyo haitakuwa na nafasi ya kupokelewa.

Akitoa Mada ya Namna Bajeti zitakazo tayarishwa kuzingatia suala zima la Usawa wa Kijinsia. Afisa Bajeti Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Mwanakhamis Mzee Hafidh amesema kumekua na Utayarishaji wa Bajeti wa Kimazoea kwa muda mrefu usiozingatia Kipaumbele cha masuala ya Usawa wa Kijinsia jambo lililopelekea Kuachwa nyumba kwa jinsi moja dhidi ya nyengine. Jambo hilo amesema Serikali imeliona na kwenye bajeti ya 2025/ 2026 watahakikisha linazingatiwa ili kujenga Jamii yenye Usawa wa kijinsia.

Ametolea Mfano wa uwepo wa Idadi kubwa ya Wasarifu Majengo na Wakandarasi wa kiume ukilinganisha na wa kike jambo linalopelekea kuachwa nyuma mno kwa jinsia ya kike kwenye miradi mingi inayoendelea nchini.

Mwanakhamis amewataka washiriki kuhakikisha wanatoa kipaombele kwa kila Kada kujitokeza kwa masuala ya usawa wa kijinsia katika utayarishaji wa bajeti zao.

Kwa Upande wake Fatma Mgeni Kombo  Afisa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango amezungumzia namna nzuri ya Uandaajibwa MTEF na PBB kwa taasisi na kuzitaka zijielekeze kwenye kuimarisha maeneo hayo kwa Taswira Njema ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Mafunzo hayo ya siku Moja Yamefungwa Rasmi na Afisa Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa niaba ya Mkurugenzi, Sera, Mipango na Utafiti wa Wizara hiyo Bi.Zahra Nassor Said na kuzishirikisha taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Unguja na Pemba .





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...