Addis Ababa, 13 Februari 2025.

 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshinda nafasi mbili zilizokuwa zikigombewa katika uchaguzi wa Taasisi za Umoja wa Afrika ambazo ni nafasi ya Mjumbe wa Tume ya Umoja wa Afrika inayohusiana na Sheria za Kimataifa iliyokuwa ikigombewa na Prof. Kennedy Gastorn na nafasi ya Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika dhidi ya Rushwa iliyokuwa ikigombewa na Bw. Benjamin Kapera.

 

Prof. Kennedy Gaston ameshinda kura 45 kati ya 48 na Bw. Benjamini Kapera ameshinda kwa kura 33 kati ya 48 zilizopigwa na kikao cha 46 cha Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika na kuibuka washindi katika nafasi husika.

 

Uchaguzi huo umefanyika tarehe 13 Februari, 2025 wakati wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya nyaraka za Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika tarehe 15 na 16 Februari, 2025.

 

Zoezi la uchaguzi huo lilienda sambamba na kunadi wasifu na uwezo wa wagombea kiutendaji ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA), Mhe. Innocent Shiyo waliongoza mchakato huo.

 

Wajumbe hao walioshinda watawakilisha kanda ya Mashariki wakiungana na wajumbe wengine kutoka katika kanda za Magharibi, Kaskazini, Kusini na Kati katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo. Nafasi ya Ujumbe wa Tume ya Sheria za Kimataifa ni miaka mitano (5) na ujumbe wa Bodi ya Masuala ya Rushwa ni miaka (6).

 

Pamoja na nafasi hizo Waziri Kombo ametumia pia fursa ya kikao hicho cha Mawaziri kumnadi mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani - Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janab.

 

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...