Na mwandishi Wetu

NAIBU  Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, amekagua na kufurahishwa na Utekelezaji mkubwa uliofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Manispaa ya Iringa Kwa kukamilisha Ujenzi wa kivuko muhimu cha waenda kwa migui kinachotumiwa na wananchi katika Kata ya Kitwiru ndani ya manispaa hiyo.

Akiwa katika kivuko hicho cha waenda kwa miguu katika hiyo,Naibu Waziri Sangu amesema kilichomfurahisha zaidi ni kusikia  kuwa asilimia kubwa ya mahitaji ya kivuko hicho cha waenda kwa miguu ujenzi wake kuanzia mchanga,kokoto na mawe vimenunuliwa kutoka Kwa Wanufaika wa TASAF.

Ambapo kupitia vikundi vyao wanufaika hao wa TASAF walikiwa wakifanya uzalishaji huo kama njia ya kujipatia kipato kuendesha maisha yao ya kila siku nje ya fedha wanazopokea kutoka TASAF kusaidia kaya masikini huku akitumia nafasi hiyo kueleza kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo hilo ni muhimu na sasa wananchi wanafurahia kukamilika kwake.

Awali wananchi wa Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa wameeleza hapo awali hasa katika kipindi cha mvua, watoto mpaka watu wazima walikuwa hawawezi kuvuka eneo hilo jambo ambalo lilikuwa linakwamisha shughuli nyingi za uchumi.

Wamesema hali iliyosababisha baadhi ya Wananchi kukosa huduma na mahitaji ya msingi ya kila siku huku Wanafunzi wakishindwa kwenda Shule na wengine kushindwa kurudi nyumbani kwasababu njia ilikuwa haipitiki kabisa.

Baada ya Kutembelewa na Naibu Waziri huyo, Wananchi hao wameishukuru TASAF huku wakieleza furaha yao kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa kivuko hicho kwani hatua kubwa ya kimaendeleo na ni mkombozi kwa kuwa limefungua mawasiliano.

Wananchi hao wamesema kwa sasa hawwna wasiwasi tena hata ikifika kipindi cha mvua njia hiyo itakuwa inapitika na kutumiwa na watu wote wakubwa na wadogo.















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...