MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendesha mafunzo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo juu ya shughuli zinazofanywa na Mamlaka.
Mafunzo hayo yamefanyika makao makuu ya mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam, leo Februari 11, 2025.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Salim Msangi, amesema ni muhimu kwa wajumbe wa Bodi ya TCAA kupata mafunzo hayo lengo likiwa ni kuwa na uelewa mpana na wa pamoja juu ya shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka.
"Kupitia mafunzo haya, wajumbe wa bodi itawasaidia kuwa na majibu ya maswali popote pale panapohitajika kujibu hoja mbalimbali," alisema Bw.Msangi.
Aidha, kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, amemshukuru Mkurugenzi Mkuu na watoa mada katika mafunzo hayo na ameshukuru kwa mafunzo hayo na kueleza kuwa ni mafunzo muhimu wa wajumbe na watumishi kwa ujumla, kwa sababu Dunia inaenda kasi kwa upande wa teknolojia hivyo ni muhimu kupata mafunzo ya mara kwa mara ili kwenda na mabadiliko yanayoendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...