

Na Mwandishi wetu - Iringa.
Wakurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ngazi ya wizara wamekutana leo tarehe 12 Februari 2025 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa lengo la kupitia Taarifa ya Utendaji wa Serikali (Government Performance Report kwa Mwaka wa Fedha 2023/24).

Kikao kazi cha wakurugenzi hao kimeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini na Maafisa kutoka katika Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini ndani ya wizara.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. James Henry Kilabuko, Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Sakina Mwinyimkuu amesema, jukumu la Ufuatiliaji na Tathmini ni muhimu katika kuboresha utendaji wa serikali kwa ujumla hivyo Serikali imeendelea kutoa msukumo na kuboresha Miundo na Mifumo kwa kuandaa Miongozo ya Ufuatiliaji na Tathmini Ili kuimarisha U&T ndani ya Serikali.



Aidha, Bi. Sakina amewaasa wataalam kutofanya kazi kwa mazoea, uoga au kutojiamini, kwani kwa kufanya hivyo serikali haitafikia malengo na kupunguza umuhimu wa kuanzisha Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini. Hivyo ni vema kuifanya ufuatiliaji na tathmini kuwa nyenzo ya msingi ya kusaidia utendaji wa taasisi, sekta na nchi kwa ujumla.

Kikao kazi hicho pamoja na mafunzo ya namna ya matumizi ya Miongozo ya Ufuatiliaji na Tathmini (U&T) katika taasisi za serikali iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kitafanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 12 hadi 13 februari 2025.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...