Na mwandishi wetu,Michuzi Blog

SERIKALI imeombwa kuingilia kati ili waliokuwa wafanyakazi pamoja na wateja wa Benki ya FBME wapate haki zao ikiwemo fedha ambazo wanaidai benki hiyo ambayo imesitisha kutoa huduma tangu mwaka 2017.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo ambapo wamedai wamekuwa wakipigania haki yao muda mrefu bila mafanikio,hivyo wanaamini Serikali ndio inayoweza kusaidia wapate haki zao.

Akizungumza kwa niaba ya waliokuwa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo leo Februari 6,2025 jijini Dar es salaam, Dk.Majura Mfungo (mteja)amesema wameamua kutoa kilio hicho ili kupaza sauti zao kwa serikali kuona namna ya kuwasaidia.

Amesema kuwa wanapitia mateso ambayo hayawahusu kwani wao walikuwa wateja na wafanyakazi katika benki hiyo hivyo pamoja na mambo mengine hawastahili kupata adhabu wanayoipita kutokana na kufungwa kwa benki hiyo

Ameongeza wafanyakazi na waliokuwa wateja wa benki hiyo walikuwa zaidi ya 100 na fedha wanazodai ni karibia Sh.bilioni 33 za kitanzania ambapo ndani ya fedha hizo kuna madai ya mafao na fedha za wateja.

"Haya madai ya fedha ambayo tumeyaeleza ni sisi tu hapa kwetu ndio hatujapata fedha zetu japo kwa sehemu walipewa kama asilimia fulani tu lakini waliowengi wanadai hadi leo na kwa upande wa matawi mengine yalioko nje ya Tanzania wenzetu wameshalipwa kwani hakuna anayedai,”Dkt Mfungo

Amefafanua licha ya kufanya jitihada mbalimbali za kutafuta haki yao ikiwemo kuandika barua na kupeleka serikalini lakini hadi leo hakuna kinachoendelea,hivyo wameamua kuiomba Serikali kuwasaidia kupata haki zao.

Amefafanua kuwa kupitia changamoto hiyo baadhi ya wafanyakazi na waliokuwa wateja wa banki hiyo wanapitia maisha magumu na wengine sasa ni wagonjwa ,huku wengine wakiwa wamepoteza hadi maisha yao bila kupata stahiki zao.

Dkt Mfungo ameongeza kuwa baada ya banki hiyo kufungwa yapo maelekezo yalitolewa ili wafanyakazi na wateja wapate stahiki zao lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na hawajui hatma yao.

"Tunaiomba Serikali itusaidie kwani maisha tunayopotia ni magumu na hapa ninapozungumza baadhi ya wenzetu wamepooza hadi baadhi ya viungo vyao. (stroke).Ni miaka nane sasa imepita ukimya umetawala licha ya kuandika barua hizo kwenda maeneo mbalimbali ,hakuna majibu.”

Kwa upande wake Zuhura farisy ambaye amepata ulemavu wa miguu amesema kutokana na kukosa haki zao imesababisha wengine kupoteza maisha kutokana na kukabiliwa na msongo wa mawazo na wengine wamepooza mwili,hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia wapate haki zao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...