NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wameshauriwa kutotumia muda mwingi kuwajibu wapinzani kwani wameshapoteza dira na badala yake washuke kwa wananchi na kueleza kazi zilizofanywa na serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, Adam Best Simba alipokuwa akizungumza na wanachama na wananchi wa kata ya Uru kusini wilayani Moshi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi.
Alisema kuwa, serikali imefanya kazi nyingi ambazo wana ccm wanajuku ya kwenda kuzisemea kwa wananchi ili wasije kudanganywa na watu wasiolitakia mema Taifa.
"Wana ccm hatupaswi kutumia nguvu kubwa kuwajibu wapinzani kwani tayari wameshapotea kutokana na kazi kubwa ambazo zimefanyika kipindi hiki kila kata zimepelekwa fedha nyingi za maendeleo sasa jukumu letu ni kushuka kwa wananchi na kuwaeleza yale yaliyofanyika katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan" Alisema Simba.
Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa alisema kuwa, mpaka sasa hakuna Chama cha kukitoa CCM madarakani na hii ni kutokana na kazi kubwa ambazo zimefanyika za kuhakikisha wanawatumikia wananchi bila kujali itikadi zao.
Katika hatua nyingine Simba aliwataka wanaccm kuhakikisha wanajiepusha na makundi ya watu ambao wamekuwa wakijipitisha na kutangaza nia za kugombea nafasi mbalimbali kwani watu hao lengo lao ni kukivuruga chama na kudai kwa sasa chama kinawatambua na kuwalinda madiwani na Wabunge waliopo madarakani.
"Kama wapo wanachama wanaotaka uongozi watambue kwa sasa muda bado wawaache viongozi waliopo madarakani wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria na pindi muda utakapofika ndipo watangaze nia zao" Alisema Simba.
Aidha Mjumbe huyo aliwataka wanachama kuhakikisha wanajisajili kwa kieletroniki pamoja na kulipa Ada ili kuwa wanachama hai pamoja na kuweza kufanya maamuzi katika vikao mbalimbali vya chama.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhani Mahanyu alisema kuwa, kata ya Uru kusini ni miongoni mwa kata ambazo zimepata fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo kituo cha Afya.
Mahanyu aliwataka wananchi kuhakikisha wanailinda miradi hiyo ili iweze kudumu muda mrefu ili lengo ambalo lilikusudiwa na serikali liweze kutimia.
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Uru kusini, Wilhard Kitali alisema kuwa, lipo tatizo la ubovu wa barabara ya Mama ndizi road inayounganisha vijiji vya Rau na Kariwa na kuwaomba viongozi wa chama waweze kusaidia kutatua ubovu wa barabara hiyo ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...