Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud T. Kombo (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini, Mhe. Nicole Providoli yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 18 Februari 2025
Madhumuni ya mazungumzo hayo yalikuwa ni Mhe. Providoli kujitambulisha rasmi kwa Mhe. Waziri Kombo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Novemba 2024.
Aidha katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekata ya Afya, maji, TEHAMA, madini na ufadhili wa masomo.
Wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano katika eneo la biashara na uwekezaji kupitia Switzerland - Tanzania Chamber of Commerce (STCC) iliyozinduliwa nchini mwezi Februari 2023.
Home
HABARI
WAZIRI MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...