Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa, akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, walipokutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek, nchini Namibia, baada ya mazishi ya Rais wa Kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa hilo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, tarehe 1 Machi 2025.

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi walipokutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek, nchini Namibia, mara baada ya mazishi ya Rais wa Kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa hilo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, tarehe 1 Machi 2025.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mzee Thabo Mbeki akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi walipokutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek, nchini Namibia, mara baada ya mazishi ya Rais wa Kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa hilo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, tarehe 1 Machi 2025.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Kashim Shettima Mustapha, Makamu wa Rais wa Nigeria, walipokutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek, nchini Namibia, mara baada ya mazishi ya Rais wa Kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa hilo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, tarehe 1 Machi 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...