Na Mwandishi wetu, Babati
MAMLAKA za majisafi na usafi wa mazingira Mkoa wa Manyara, imepanga makadio ya matumizi ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2025/2026 ya shilingi 28,224,455,064.00.
Katika makadirio hayo matumizi ya uendeshaji ni shilingi 10,302,892,869.00 gharama za uwekezaji ni 507,329,245.00 na Serikali kuu shilingi 17,414,232,950.00
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kwenye mkoa wa Manyara kwa mwaka 2025/2026 ili kuhakikisha huduma ya maji inakuwa bora imekadiria kukusanya shilingi 10,810,222,114 ambazo shilingi 10,302,892,869 ni matumizi ya kawaida na shilingi 507,329,245.00 ya miradi ya maendeleo.
Pia, Mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira mkoa wa Manyara, zimeomba shilingi 17,414,232,950.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya maji Orkesumet, (Ngurash, mlima City, Lerumo na Loiborsoit).
Zimeombwa pia Kibaya mjini, Mbulu mjini , Katesh, Darakuta-Minjingu, Dareda, Gallapo, Madunga - Naar - Bashnet - Secheda - Ufana na Babati mjini.
Mkurugenzi wa BAWASA Iddi Msuya ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha ushauri kamati ya mkoa huo (RCC) kilichofanyika hivi karibuni mjini Babati.
Msuya amesema mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye mkoa wa Manyara, kuna mamlaka tatu ambazo ni BAWASA, MBUWASA na Kibaya.
Amesema BAWASA inahudumia katika Mji wa Babati na Kata 10 za Babati Vijijini, miji midogo ya Katesh Wilayani Hanang’ na Orkesumet Wilayani Simanjiro.
Amesema mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbulu (MBUWASA) inahudumia maeneo ya Mbulu mjini na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kibaya Wilayani Kiteto inahudumia Kibaya mjini.
Msuya amesema maeneo yanayohudumiwa na mamlaka hizo ni wakazi 471,152 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 ambapo watu wanaopata maji kupitia mamlaka hizo ni 403,430 sawa na asilimia 86 ukilinganisha asilimia 80, Februari 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga amepongeza utendaji kazi wa mamlaka hizo katika kutoa huduma za maji katika jamii kwenye eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...