Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kuimarisha weledi na uadilifu wa watumishi wa taasisi hiyo ambapo katika kipindi cha miaka minne imefukuza kazi watumishi 14 na kushusha mshahara watumishi 6 na kushushwa cheo na kupunguziwa mshahara watumishi 12 huku watumishi 22 wakipewa barua za onyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw, Yusuphu JumaMwenda wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Mamlaka hiyo kwa katika kipindi cha miaka mine ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Ofisi ya Idara ya Habari Maelezo Jijini Dodoma.
Kamishina amesema katika kutumia mifumo ya tehama katika usimamizi wa kodi ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya tehama mamlaka ya mapato imefanikiwa kukamilisha na kuboresha mifumo ujenzi wa mfumo wa uwasilishaji ritani kwa mtandao kwa kodi za Pay As- You-Earn (PAYE), Corporate Tax (CIT), Withholding Tax (WHT) & Skills and Development Levy (SDL).
“Ujenzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) ikiwa ni pamoja Uboreshaji wa Mfumo wa Forodha (TANCIS) katika kuboresha mfumo wa usimamizi wa kodi za forodha (TANCIS) ambao umezinduliwa na unaendelea kutumika na wadau wote na kurahisisha utoaji wa huduma za Forodha,” alifafanua
Aidha katika Kuboresha na Kuimarisha Huduma kwa Walipakodi jumla ya Ofisi mpya 40 zimefunguliwa katika maeneo ambayo awali hayakuwa na Ofisi na tumefanikiwa kukarabati na kujenga Ofisi 41 kuanzia ngazi za Mikoa, Wilaya, Vituo vya Ukaguzi (check- points) pamoja na Ofisi za Mipakani.
Pia mamlaka imeendelea kuwatambua, na kuthamini kwa kuwazawadia Walipa Kodi Bora kwa kuwatambua walipakodi hao wanaofanya vizuri na kuwazawadia kwa namna wanavyofanya vizuri nchi nzima.
Sambamba na hilo Mamlaka ya Mapato imeendelea kupambana na wakwepa kodi kwa kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi yao pamoja nakuendelea kutoa elimu ya kodi na madhara ya ukwepaji kodi.
Kamishina Alifafanua kwamba, imeendelea kupambana na wakwepa kodi kwa kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi yao pamoja nakuendelea kutoa elimu ya kodi na madhara ya ukwepaji kodi.
Katika hatua nyingine Mamalaka ya Mapato tumeendelea kubaini mianya ya upotevu wa mapato na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika. Hii imeongeza uwajibikaji na kuongeza mapato ya serikali.
Ameongeza kusema, “mianya ya ukwepaji kodi ni pamoja uwepo wa magendo kupitia mipaka yetu (uncustomed goods); Ghost receipt za EFD; Counterfeit ETS; Dumping of Transit goods; Abuse of tax exemptions; Undervaluation of imported goods. Katika miaka minne tumeweza kufungua case 77 za ukwepaji kodi katika mahakama mbalimbali pamoja na kurecover kiasi cha kodi kilichopotea.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...