Wadau mbalimbali wa maendeleo Nchini Tanzania wamekutana
jijini dar es salaam kama sehemu ya kujadili maswala mbalimbali yanayohusu
utunzaji wa viumbe hai kupitia Mradi wa Biodiversity finance initiative
uliozinduliwa jijini Dar es salaam na naibu katibu Mkuu ofisi ya makamu wa
Rais Mh. HASSAN MOHAMED HASSAN
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, ABDALLAH HASSAN
MITAWI amesema mabadiliko ya tabianchi yana mchango mkubwa katika kuathiri
viumbe hai na Mazingira nchini Tanzania ameyasema hayo katika uzinduzi wa Mradi
wa Biodiversity finance initiative ululiozinduliwa kwa mara ya kwanza Tanzania
Bara
Kwa upande mwingine mchambuzi wa programu wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) FERISTER IGNATUS amepongeza dhamira ya
Tanzania Bara katika kuunga mkono mpango wa kudhithibi uwepo wa viumbe hai na
Mazingira salama kwa jamii
HASSAN MOHAMED HASSAN ambaye ni mratibu wa BIOFIN Zanzibar
ameeleza sababu zinazopelekea Zanzibar kupata mafanikio katika mipango ya
kutunza Viumbe hai kupitia Mradi wa Biodiversity finance initiative ambapo sera
wezeshi na usimamizi mzuri zinatajwa kuwa sababu kuu za kufanikiwa kwa Mradi
huu
Mradi wa Biodiversity finance initiative unatajwa kuleta mageuzi Tanzania Bara mara baada ya kuzinduliwa kwa mara ya kwanza huku wadau mbalimbali wa maendeleo wakiunga mkono sera ya utunzaji viumbe hai
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...