NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
TANZANIA imeibuka kidedea Afrika katika uzalishaji wa kahawa bora aina ya Robusta kupitia kampuni ya Ubumwe Co.Ltd kilichopo wilayani Ngara mkoani Kagera na kuzishinda nchi za Ethiopia, Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, Zambia, Malawi na Ivoricost.
Akizungumzia ushindi huo jana, Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa nchini, Primus Kimario alisema kuwa, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa wazalishaji wa kahawa barani Afrika ambapo katika mkutano huo walishindanisha kahawa mbalimbali.
Alisema kuwa, katika mashindano hayo, Tanzania iliibuka kidedea kwa uzalishaji bora wa kahawa aina ya Robusta Afrika kupitia kampuni ya Ubumwe ambapo ni fursa na wao kama Bodi ya kahawa wanajivunia ubora huo wa kahawa.
“Zipo kampuni nyingi zilishiriki katika mashindano haya ya kahawa bora Barani Afrika na wenye mashamba makubwa walishiriki hivyo tunaendelea kutoa elimu na kuboresha kahawa zetu ikiwa ni kuwashawishi Wakulima kufuata njia nzuri” alisema Kimario.
Na kuongeza kuwa “moja ya jambo ambalo tutaendelea kuliimiza ni Wakulima kutokuchanganya kahawa kutoka amkosi moja na nyingine na kahawa ivunwe ikiwa imeiva tumeona wenzetu wengi walioshinda ni wale ambao wapo mahali pamoja wanachuma kahawa zilizoiva na kuitayarisha na maji safi na wameianika vizuri tukifanya hivo tunatunza ubora wake”.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Prof. Aurelia Kamuzora alifurahishwa kuona Tanzania imetoka kidedea kwa uzalishaji wa kahawa bora ya Robusta barani Afrika na kudai kuwa yapo mengi ya kujifunza kutoka katika kampuni ya Ubumwe.
Alisema kuwa, shida kubwa inayotokea katika kahawa hapa nchini ni kuchanganya kahawa kutoka eneo moja na jingine ambapo kitendo hicho huaribu uhalisia na ubora wa kahawa.
“ Mtu anayezalisha kahawa Karagwe anaweza kuchanganya na kahawa ya Songwe hili linachangia kuharibu ubora wake tunaenda kujipanga kuhakikisha Wakulima wetu hawachanganyi kahawa zao ili kuhakikisha kahawa inapata soko bora” alisema Prof. Aurelia.
Akizungumzia jinsi mashindano hayo yalivofanyika, Afisa Ubora na masoko Bodi ya Kahawa Tanzania, Felix Mlay alisema kuwa, zoezi la mashindano hayo lilianza mwaka jana Disemba ambapo kwa mashindano ya ndani ya nchi na sampuli 73 za kahawa kutoka kwa wazalishaji wadogo na wakubwa.
Alisema kuwa katika shindano hilo washindi walipatikana ambapo kwenda kwenye mashindano ya Afrika zilichukuliwa kahawa tano kwa ajili ya kwenda kushindanisha katika makundi matatu ambayo ni Robusta, Arabika laini na Arabika ngumu.
Aliongeza kuwa katika mashindano hayo ya Afrika kulikuwa na majaji sita kutoka katika nchi tofauti ambapo zilikuwepo sampuli 73 na Tanznaia iliibuka mshindi katika uzalishaji bora wa kahawa aina ya Robusta.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ubumwe Co. Ltd, Elisha Ntalamka alisema kuwa, sababu kubwa zilizopelekea kushinda ni kuzingatia ubora wa kahawa kwa kutoa elimu kwa Wakulima namna bora ya utunzaji na uvunaji bora wa kahawa pamoja na njia sahihi ya kutunza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...