Mapambano dhidi ya matumizi ya Nyuklia duniani kote yanaendelea, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi 178 zilizosaini na kuridhia Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya Nyuklia kati ya nchi 187 zilizotia saini mkataba huo kwa kuzingatia athari zitokanazo na matumizi ya nyuklia kwa watu na Dunia kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika mazungumzo na waandishi wa habari kufuatia kikao chake na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya Nyuklia (Comprehensive Nuclear-Test-Ban Treaty-CTBTO), Dkt. Robert Floyd amezisihi nchi zilizosalia kuweza kutilia saini mkataba huo wenye lengo la kulinda amani na usalama wa kila mtu duniani kote.

 

Kwa upande wake Dkt. Floyd ameipongeza Tanzania kwa kuwa kinara katika kujenga na kuilinda amani na usalama duniani ikiwa ni pamoja na kupinga matumizi ya nyuklia duniani.

 

“Tanzania si maneno tu bali vitendo, Tanzania haina tu diplomasia nzuri bali ina utajiri wa ujuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Kwa niaba ya nchi 187 wanachama wa CTBTO shukrani kwa Tanzania kuwa na mchango mkubwa katika amani na usalama duniani.

 

Akiwa nchini kwa ziara ya siku mbili iliyoanza Februari 27, 2025, Dkt. Floyd ametembelea atatembelea Kituo cha Ung’amuzi wa Viashiria vya Majaribio ya Silaha za Nyuklia kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chenye uwezo wa kung’amua viashiria vya majaribio ya silaha za nyuklia kwa njia ya hewa na kutoa mhadhara kwa umma kuhusu “Kudumisha mafanikio ya CTBTO katika kipindi cha mabadiliko duniani.”

 

Aidha, ametembelea ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania zilizopo Mbezi Msakuzi ambapo ameipongeza TAEC kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo kipya cha ung’amuzi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...