Katika kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inaleta tija kwa wananchi wilayani Ilala, Mkoani Dar es salaam, Mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo ameagiza viporo vyote vikamilike. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala, ametoa wito huo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye sekta ya Afya, elimu na miundombinu ya barabara. 

Akiwa katika mradi wa kituo cha afya Mvuti, Mpogolo amepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kituo kilichojengwa kwa thamani ya shilingi miliini 500 kutoka  kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es salaam Zaituni Hamza.

Ambaye ameeleza maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya mradi ambao una lengo la kusogeza huduma ya afya karibu na kupunguza msongamano katika vituo na hospital za rufaa pindi utapoanza kutumika. 

Miradi mingine aliyokagua Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kupokea taarifa ni sekta ya elimu ya sekondary ambapo ameagiza hadi ifikapo  april mosi mwaka huu shule hizo zianze kupokea wanafunzi. 

Mpogolo ametoa maagizo hayo kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigenzi chini na  Mkuu wa Sekomdari Yongwe ambazo ujenzi wa shule hizo  umevuka asilimia 90. 

Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Yongwe Carl Chiwangu ameeleza mradi huo ulipokea fedha milioni 350  chini ya miradi ya Kishindo cha Mama. 

Fedha ambazo zimetumika kujenga Madarasa 6,  ofisi 2 ,  maabara, na jengo la utawala, pamoja na miumdombinu mingine.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo , amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Elihuruma Mabelya kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha miradi yote iliyokwama inakamilika na kuanza kutumika kwa wakati.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...