Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Vodacom imezindua duka jipya la huduma kwa wateja kata ya Nungwi, mkoa wa Kaskazini A, ikiwa ni hatua muhimu ya kutoa huduma bora za mawasiliano na bidhaa za kisasa kwa wakazi wa eneo hilo. Duka hilo lilizinduliwa rasmi na Katibu Tawala wa mkoa wa Kaskazini A, Mariam Khamis, akishuhudiwa na mdau wa Vodacom Saleh Judas na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo Brigita Shirima. Uzinduzi ni hatua mojawapo ya Vodacom kupanua huduma zake visiwani humo ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...