MAKAMU Mwenyekiti wa Chana Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewahakikishia wananchi wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga Chama hicho kitaendelea kutatua changamoto zao ikiwemo ya kuhakikisha wanapata mazao mengi ya kilimo kwa kusambaza pembejeo na kujenga miundombinu muhimu.

Wasira ameeleza hayo leo Machi 28, 2025 alipokuwa akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM wilayani humo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 na kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara mkoani Shinyanga.

Wasira alihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Shinyanga na kuanza ziara kama hiyo mkoani Simiyu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...