WAKAZI
wa nne Same mkoani Kilimanjaro wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Moshi wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya
kukutwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi ya jumla ya kilogramu 518.57.
Katika
hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Machi 28,2025 na
wakili wa serikali Julieth Komba imewaja washtakiwa hao kuwa ni Nimkaza
Mbwambo, Prosper Lema, Nterindwa Mngalle maarufu kama mama Dangote na
Stephano Mrutu.
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ally Mkama ambapo kila mmoja amesomewa kosa lake.
Mshtakiwa
Nimkaza anadaiwa kukutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi
zenye uzito wa kiligramj 138.58, Machi 21, 2025 huko katika kijiji cha
Rikweni Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Mshtakiwa Prosper
Lema yeye anadaiwa kuwa siku na mahali hapo alikutwa akisafirisha
kilogramu 113.29 za dawa za kulevya aina ya Mirungi
Mshtakiwa
Nterindwa Mngalle anadaiwa Machi 21,2025 huko katika kijiji cha Rikweni
Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro alikutwa akisafirisha dawa za kulevya
aina ya Mirungi zenye uzito wa kilogramu160.25.
Naye mshtakiwa
Stephanie Mrutu amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkama
kujibu shtaka la kukutwa na kilogramu 106.45 za dawa za kulevya aina ya
Mirungi.
Wakati huo huo, washtakiwa wawili, Dorisiana Mchome na
Aisha Mbaga wa Same, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same
wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi
zenye uzito wa kilogramu 54.15
Washtakiwa wamesomewa kila mmoja
shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Hozza ambapo wanadaiwa kutenda
kosa hilo Machi 21, Huko Rikweni kata ya Tae wilaya ya Same mkoani
Kilimanjaro.
Wakili wa serikali Michael Matowo amedai siku na
mahali hapo mshtakiwa Dorisiana alikutwa akisafirisha kilogramu 17 za
dawa za kulevya aina ya Mirungi huku mshtakiwa Aisha Mbaga akidaiwa
kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi yenye uzito wa kilogramu
37.15
Hata hivyo washtakiwa waliofikishwa katika mahakama ya
Moshi wamerudishwa rumande hadi Aprili 11 mwaka huu kesi hiyo
Itakapokuja kwa ajili ya kutajwa wakati washtakiwa walifikishwa mahakama
ya Same wamerudishwa rumande hadi Aprili 10,mwaka huu
Hivi
karibuni Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)
ilifanya operesheni maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, ambapo
ekari 285.5 za mashamba ya mirungi ziliteketezwa. Katika operesheni
hiyo, mfanyabiashara Interindwa Kirumbi, maarufu kama Mama Dangote,
alikamatwa pamoja na wenzake kwa tuhuma za kujihusisha na biashara
haramu ya mirungi. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa katika biashara
hiyo kwa zaidi ya miaka 30, akisimamia mitandao ya usambazaji wa mirungi
nchini.
Serikali, kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya na
Wizara ya Kilimo na Mifugo, imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu
madhara ya mirungi na kuwawezesha kujikita katika kilimo cha mazao
mbadala na ufugaji. Miradi kama ufugaji wa nguruwe na miche ya kahawa
imeanzishwa ili kuwasaidia wakulima kuachana na kilimo cha mirungi.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesisitiza kuwa operesheni
dhidi ya biashara ya mirungi itaendelea ili kuhakikisha inatokomezwa
kabisa nchini.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...