Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Antonie Tshisekedi ambaye pia ni  Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Therese Kayikwamba Wagner amewasili nchini.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Mhe. Wagner amelakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo.

Akiwa nchini Mhe. Wagner anatarajia kuwasilisha ujumbe maalum wa Mheshimiwa Rais Tshisekedi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Therese Kayikwamba Wagner akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Waziri wa mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Therese Kayikwamba Wagner (kushoto) amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...