Wizara ya Fedha imeungana na washiriki wengine katika kutoa elimu kwa umma kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kitaifa jijini Arusha. Maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufikia kilele siku ya tarehe 8 Machi, 2025, Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Maonesho hayo yana kauli mbiu ‘’Wanawake na wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’’.
Maafisa Hesabu Wakuu, Kitengo cha Huduma za Mfuko Mkuu (CFS), Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky na Bi. Mercelina Haule, wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani, yanayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amiri Abeid, jijini Arusha, yenye kauli mbiu ya ‘’Wanawake na wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’’.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...