Kampuni mashuhuri ya kitalii ya nchini Tanzania ZARA TANZANIA ADVENTURES imetoa mchango wa madawati katika shule ya msingi Kaloleni iliyopo wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
Mchango huo ni moja ya mafanikio ya hamasisho la kampeni ya Twenzetu Kileleni msimu uliopita wa 2024. Hivyo Zara Tanzania Adventure imeendelea kuwa kinara katika utoaji wa huduma za kitalii nchini Tanzania hususani katika safari za upandaji Mlima Kilimanjaro na safari za Hifadhi za Taifa, kwa wageni mbali mbali wanaofika kutoka mataifa mbalimbali na watalii wa ndani.
Zara Tanzania Adventure, ambayo imeendelea kuwa kinara katika mfululizo wa ushindi wa Tuzo za Utalii Duniani yaani World Travel Awards, sasa Zara imeingika katika kinyang'anyiro hicho tena kwa msimu wa 2025.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...