NA SAID MWISHEHE, MICHUZI TV
WADAU wa mazingira nchini wamesema umefika wa kutengenezwa sera na miongozo ambayo itaongoza wawekezaji wenye viwanda vya kuchakata betri chakavu zenye asidi ya risasi(Lead Acid)kutekeleza shughuli zao bila kuhatarisha mazingira au changamoto za kiafya.
Wametoa ushauri huo leo April 10,2025 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa mazingira ambacho kimeandaliwa na Taasisi ya AGENDA na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Lengo la kikao hicho pamoja na mambo mengine limepitia muongozo wenye lengo la kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa kuondoa betri chakavu ambapo wadau baada ya kujadiliana kwa pamoja watatoka na muongozo ambao utatumiwa nchini kukomesha taka zinazotokana na betri chakavu.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao hicho Kaimu Meneja wa Mapitio ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kutoka NEMC Mhandisi Luhuvilo Mwamila amesema kuna haja ya kuwa na muongozo wa pamoja utakaowezesha kutumiwa katika kudhibiti taka za betri chakavu ambazo ziko kwa wingi mtaani.
“Hakuna miongozo rasmi ambayo ipo katika miradi hii lakini kwa sasa iko miongozo ambayo inazungumzia kwa ujumla wake , hivyo tunahitaji miongozo maalumu itakayotumika kudhibiti taka zinazotaka na betri zenye asidi ya risasi.
Akieleza kuhusu warsha hiyo amesema imehusisha wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za wasimamizi wa sera,wachakataji wa vibali na wasimamizi wa sheria mbalimbali kwa ajili ya kujadili namna bora itakayoweza kuviongoza viwanda vya kuchakata taka za betri chakavu za lead Acid ili vifuate sheria.
“Viwanda hivi vina changamoto ya uchafuzi wa mazingira lakini vinahatarisha afya kwa jamii na wafanyakazi wa viwanda pale ambapo vinakuwa havizingatii sheria lakini pamoja na kuwa na changamoto hizo tunavihitaji hivi viwanda kwasababu nchi inakuwa na uchumi unaokua, na hii iko kote kidunia.
“Magari yanaongezeka nchini na magari ndio chanzo kikubwa cha aina hii ya taka.Pia uzalishaji wa umeme jua nao unatumia aina hii ya betri za lead acid, kwahiyo tunahitaji viwanda hivi lakini tunapaswa kudhibiti taka hizi ambazo tunazizalisha sisi wenyewe,”amesema.
Amefafanua siku za karibuni nchi za Afrika walikuwa na mkutano wa kikanda wapamoja nan chi hizo zimepata nafasi ya kuelezea jinsi ambavyo hali ya viwanda vya aina hiyo ilivyo katika nchi zao na imeonekana kote zinafanana.
“Katika mkutano ule tumeona tukae pamoja na kutengeza miongozo ya aina moja itakayosimamia wawekezaji wa viwanda vya kuchakata betri chakavu ambao wengi wanatoka nchi nyingine , tukiwa na muongozo wa pamoja na tukaweka viwango basi itawezesha wawekezaji hao katika nchi yoyote watakayokwenda kufuata miongozo hiyo.”
Kwa upande wake Angella Kilio ambaye ni Mwanasheria wa NEMC amesema wao kama Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira wanafahamu suala zima la kuondosha mabetri yaliyotumika katika mazingira yetu vinawahusu kwa ujumla kuanzia namna ya kukusanya, kusafirsisha na kuhifadhi huku akisisitiza sheria na kanuni za taka hatarishi zipo na zinatakiwa kufuatwa.
“Kanuni zipo lakini tunayo sheria mama ya mazingira na ziko wazi na zimeelezea vizuri…kwamfano mtu anayeshughulika na taka hatarishi kanuni inaeleza anayeharibu mazingira anapaswa alipie .Sheria inaeleza namna gani ya kuomba kibali kama cha chini ya tani tano , uwe na leseni pamoja na TIN.
“Ujumbe wetu kwa watanzania ni kwamba kutokana na matumizi ya betri yamekuwa makubwa hivyo betri chakavu zimekuwa nyingi mtaani tunaomba hizo taka watumie kama fursa lakini katika namna ambayo mazingira yetu yatalindwa na afya zetu zitabaki salama.”
Awali Ofisa Programu Mkuu Silvani Mng’anya kutoka Taasisi ya AGENDA amesema wadau hao wamekutana kwa ajili ya kuangalia changamoto ya urejereshaji wa taka za betri chakavu.
“Kwahiyo tumeandaa mpango wa kuutekeleza katika kupunguza tatizo la uwepo wa taka za betri chakavu. Oktoba mwaka 2024 tulikutana na tuliona jinsi viwanda vinavyofanya kazi…
“Lakini mazingira ya viwanda hivyo yameonesha kuna haja ya kuchukua hatua ili kuboresha mazingira na kuwa bora kwa kurejeresha betri chakavu ili kuepuka athari za betri hizo kutokana na hali iliyopo sasa hivi.
“Kwahiyo tumekutana ili kupitia rasimu ya muongozo wa utekelezaji na tutakubaliana hatua za kuchukua kama wadau kwa kuwa na muongozo tutakaotumia nchini kwetu.”
Kuhusu nafasi ya Taasisi ya AGENDA katika kutomeza taka za betri chakavu amesema mpango wao mkubwa ni kukusanya wadau kama ambavyo wamefanya leo kwa ajili ya kufanikisha kuandaa muongozo utakaotumika kudhibiti taka za betri .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...