Watumishi wa TPDC na GASCO katika picha ya pamoja wakati wa kupokea tuzo
Kampuni ya GASCO, ambayo ni kampuni tanzu ya TPDC, imepokea tuzo nne (4) kwa niaba ya viwanda vya kuchakata gesi asilia vya Madimba na Songosongo, pamoja na Kituo cha Kupokea Gesi Asilia cha Kinyerezi, sambamba na tuzo ya heshima kwa udhamini.
Tuzo hizi zilitolewa mbele ya Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), ikiwa ni kutambua mafanikio ya GASCO katika kuzingatia viwango bora vya afya na usalama kazini.
Tuzo hizo zimetolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) katika maonesho yaliyofanyika kitaifa na kushirikisha makampuni kutoka sekta mbalimbali. Ushindi huu umeweka alama ya kipekee kwa GASCO kama kinara katika utekelezaji wa sera na taratibu bora za usalama kazini.
Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa GASCO, Ndg. Msaada Elson akipokea tuzo
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Meneja Mkuu wa GASCO, Ndg. Msaada Elson alieleza kuwa ushindi huo ni matokeo ya mshikamano, uwajibikaji na juhudi za pamoja kati ya menejimenti na wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.
“Ushindi huu ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya menejimenti na wafanyakazi wote katika kuzingatia viwango bora vya afya na usalama kazini. Kampuni itaendelea kuboresha mifumo ya usalama na kutoa kipaumbele matumizi ya akili mnemba kwa ustawi wa wafanyakazi wake,” alisema Ndg. Msaada Elson.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwashukuru OSHA kwa kuandaa maonesho hayo ambayo yanatoa jukwaa muhimu kwa makampuni kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za usimamizi wa usalama kazini.
Tuzo hizo zinaonesha dhamira ya dhati ya GASCO katika kuhakikisha mazingira salama kwa wafanyakazi, kuongeza tija kazini na kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya nishati nchini.
#TPDCTUNAWEZESHA
PICHA A: Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa GASCO, Ndg. Msaada Elson akipokea tuzo
PICHA B: Watumishi wa TPDC na GASCO katika picha ya pamoja wakati wa kupokea tuzo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...