UONGOZI wa Kiota cha Maraha cha Lizy Park umeandaa Tamasha Maalum linalolenga kusaidia Watoto Yatima na Wazee wasiyojiweza Aprili 25, 2025 kilichopo Sinza Lion jijini Dar es Salaam.

Kati ya bendi hizo zitazotumbuiza ni pamoja na bendi ya RTS (Kihangaiko), Ruvu Star's, Mbweni JKT na Sikinde OG, ambapo kati ya bendi hizo tatu zikiwa za Jeshi na moja ikiwa ya uraiani, zitatumbuiza huku mshindi wa kwanza akiondoka na zawadi ya kiasi cha Shilingi Mil2, wa pili Mil1 na watatu 500,000.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Lizy Park, Elizabeth Chacha, amesema lengo la kuandaa tamasha hilo ni kurudisha kwa jamii, akieleza kuwa kiasi kitakachopatikana kwenye tamasha hilo chote kitapelekwa wahitaji hao.
"Lengo la kuandaa tamasha hili kumetokana na kutambua kurudisha kwa jamii inayotuzunguka, kama tunavyojua kuwa wapo watu wengi wenye uhitaji maalum na hawana pa kukidhi mahitaji yao, hivyo Lizy Park tumeona ni vyema kupitia Sherehe hizi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tukaadhimisha kwa kujitolea kwa jamii yenye uhitaji" amesema Elizabeth.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo, Cecilia Jeremiah ametoa wito kwa wadau wote wa mziki wa dansi kuhudhuria kwa wingi, ili kuunga mkono juhudi hizo ikiwa pamoja na kupata burudani kutoka kwa magwiji hao wa muziki wa dansi.

"Siku hiyo siyo ya kukosa ni vyema watu wote hususan wadau wa mziki wa dansi kujitokeza kwa wingi, wengi wetu hawajui kama bendi za Jeshi zinafanya vizuri hivyo ni muhimu kutumia siku hiyo kujitokeza kwa wingi kuja kuzishuhudia bendi hizo zinavyofanya vizuri...niwahakikishie tu kuwa burudani itakuwa ya kukata na shoka hivyo usikubali kukosa", alisema Cecilia.

Kiota cha Lizy Park kipo maeneo ya Sinza Lion zamani pakijulikana kama T Galden na kiingilio kitakachonogesha burudani hiyo ni Shilingi 10,000 ambayo mhusika atapatiwa na bia 2.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...