Katika kuadhimisha Maonesho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Akiwa banda la TCAA , Mheshimiwa Hemed alipata maelezo kuhusu huduma na majukumu ya TCAA pamoja na miradi inayoitekeleza kutoka kwa Meneja wa Kituo cha TCAA katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA), Bw. Mohamed Ali Mohamed.

Katika maelezo yake, Bw. Mohamed pia alimueleza Mheshiwa Hemed namna TCAA inavyosimamia usalama wa safari za anga, kuratibu huduma za Uongozaji ndege, pamoja na kuendeleza teknolojia za kisasa kuhakikisha kunakuwa na ufanisi na maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini na visiwa vya Zanzibar kwa ujumla.

Mheshimiwa Hemed alipongeza jitihada za TCAA katika kuimarisha huduma za usafiri wa anga na kuhimiza mamlaka hiyo kuendelea kuboresha huduma kwa maslahi ya taifa na wananchi.

Maonesho hayo ya Mei Mosi yanazileta pamoja taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi kuonesha huduma na mafanikio yao katika kuunga mkono maendeleo ya kitaifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha TCAA katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA), Mohamed Ali Mohamed kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...