NA. MWANDISHI WETU BERLIN, UJERUMANI
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bi. Gérardine Mukeshimana, katika kikao cha pembezoni mwa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Watu Wenye Ulemavu uliofanyika tarehe 2–3 Aprili, 2025 mjini Berlin, Ujerumani.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Ummy amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendeleza ushirikiano na IFAD katika kuimarisha miradi ya kilimo inayolenga kuwawezesha watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa maendeleo jumuishi.
Viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya maendeleo jumuishi ili kuhakikisha programu za kilimo zinakuwa shirikishi, zenye usawa, na zenye manufaa kwa jamii nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...