Na Mwamvua Mwinyi, Mafia April 8,2025


Mwenge wa Uhuru umetembelea ,kukagua na kuweka jiwe la msingi miradi 15 yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 2.8 .

Akipokea mwenge wa Uhuru Aprili 7, 2025, kwa mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo amesema kati ya miradi hiyo 11 imekaguliwa, miradi mitatu imezinduliwa, na mradi mmoja umewekewa jiwe la msingi, kwa umbali wa kilomita 64.9 .

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi, ameonyesha kuridhishwa kwake na kupongeza usimamizi na utekelezaji wa miradi wilayani Mafia.

Alisisitiza kuendeleza uzalendo kwa kufanya kazi kwa bidii na amewahimiza wananchi kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.

" Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na utekelezaji wa miradi wilayani hapa, uuendelee kutunza miradi hii maana inatekelezwa kwa fedha nyingi. "

"Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunaishi maisha bora yanayofanywa na Serikali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan," alisema Ussi.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa wilayani BagamoyoAprili 8, 2025.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...