ZAIDI Ya Wachezaji 120 wanatarajiwa kushiriki shindano la siku moja la CRDB Coastal Zone Inter Club lenye lengo la kujenga ushirikiano mwa klabu za gofu za ukanda huo

Nahodha Msaidizi wa klabu ya gofu ya jeshi la wananchi JWTZ ya Lugalo ya jijini Dar es salaam Kapteni Samwel Mosha amesema kwenye shindano hilo watacheza Mchezaji mmoja mmoja badala ya kucheza kitimu

Aidha Kapteni ameongeza Kuwa timu zitakazoshiriki katika shindano hilo ni pamoja na Dar gymkhana,Moro Gymkhana na pamoja na Wenyeji wa shindano hilo Lugalo gofu .

Mkuu wa wateja binafsi benk ya CRDB Steven Adil amesema Watanzania wanashiriki michezo kwa lengo la kujenga afya na kufanya michezo kuwa ajira hasa katika mchezo huo ambao umeanza kukubarika kwenye jamii.

Kwenye shindano hilo la CRDB COASTAL zone Inter Club linatarajiwa kushirikisha wachezaji kutoka katika klabu tatu za mkoa wa Dar es salaam ikiwemo klabu ya gofu ya Lugalo na Gykhana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...