Na Mwandishi Wetu, Songea
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema umekamilisha maandalizi ya kuanza kutekeleza Bima ya Afya kwa Wote ambapo imewaomba wananchi kuendelea kujiunga na vifurushi ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Hipoliti Lello wakati akiwasilisha mada juu ya utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote kwenye Mkutano Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Alisema kuwa Baada ya kupitishwa na kuanza kutumika kwa baadhi ya vifungu vya Sheria hiyo namba 13 ya mwaka 2023, Mfuko umefanya maandalizi ya kuhudumia wananchi wengi zaidi ambapo imeimarisha Mifumo ya TEHAMA ambapo kwa sasa wananchi wanaweza kujihudumia popote walipo kwa njia ya mtandao.
“Maandalizi yaliyofanyika ni pamoja na kuandaa vitita vya mafao, kuwezesha matumizi ya mifumo hususan usajili, ulipaji michango, utambuzi wa wanachama, uwasilishaji na uchakati wa madai ambao kwa sasa unafanyika kidijitali,” alisema Bw. Lello.
Alisema kuwa Mfuko umeendelea na ushirikishaji wa wadau ili kupata maoni ya namna bora ya utekelezaji hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba Wahariri kuendelea kushirikiana na Mfuko katika kuelimisha wananchi ili wachukue hatua ya kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu bila kikwazo cha fedha.
Mkutano huo wa Wahariri ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye alisisitiza umuhimu wa vyombo vya Habari katika kukuza maendeleo ya nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...