Na Mwandishi Wetu.

MWALIMU wa Shule Binafsi Irene Muthemba amesema Shule ya Ukonga Skillful imebeba siri kubwa na shuhuda za mafanikio ya vijana wengi hasa waliokuwa wamekata tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Muthemba alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mahafali ya 19 ya wanafunzi kidato cha sita wanaohitimu katika shule hiyo,alisema kwa muda mfupi aliokaa katika eneo amebaini mambo makubwa kuhusu shule hiyo kuhusu walimu na wanafunzi.

"Ningeambiwa niandike chochote kuhusu hii shule,ningesema kuwa ina siri kubwa na shuhuda nyingi sihitaji kuambiwa lakini ukiona watu wa hapa inaonyesha kuna shuhuda nyingi na siri kubwa mpaka wahusika wanafika hapa na wengine waliofanikiwa kwakupita hapa,"alisema Muthemba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Alisema pamoja na wanafunzi kusoma kwa bidii lakini walimu wa shule hiyo wanachukua nafasi kubwa katika kuwasimamia wanafunzi.

"Mimi ni mwaalimu wa miaka mingi uzoefu wangu ni miaka 12 na nusu,hii kazi siiifanyi tu kwa sababu ni mwaalimu,naomba niwakumbushe walimu wenzangu kuwa katika huduma za Mungu ualimu ni huduma ndo maana Mungu anatubariki.

"Walimu wa hii shule nawashukuru sana kitu cha kwanza nilichokiona ni nidhamu za wanafunzi,tangu nimekaa hapa naona watoto wametulia sio kawaida kundi lote hili kusiwe na hata na drama mnafanya kazi kubwa sana,"alisema Muthemba.

Aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii bila kukata tamaa na kwamba wapambane mpaka kieleweke.

Naye muasisi wa Ukonga Skillful Diodorus Tabaro alisema jumla ya wanafunzi 78 ambao wanatarajiwa kuhitimu kidato cha sita wametunukiwa vyeti katika mahafali hayo ambapo kati ya wanafunzi 72 ni kutoka makao makuui na wanafunzi sita wanatoka tawi la shule hiyo lililopo Mbezi Luis.

"Wanafunzi wanaohitimu Leo (juzi) ni wale waliosoma kidato cha tano na sita kwa mwaka mmoja,ni muendelezo wa shule hii katika kutoa wahitimu ambao ni kundi la watu waliokuwa wamekata tamaa yakuendelea na masomo.

"Vijana kama walihitimu kidato cha sita mwaka jana walikuwa 52,ninachokumbuka asilimia 98 ya Vijana nao walijiunga vyuo vikuu na wamepata mkopo.hivyo matokeo tuliyoyapata mwaka jana na mwaka huu tunaomba tuyapate kama hayo,"alisema Tabaro.

Alisema mahafali ya 19 ni ishara yakuelekea miaka 20 ya kuanzishwa kwa shule hiyo ifikapo mwakani.

"Haya ni mhafali ya 19,tulianza safari yetu kwa wanafunzi wenye ndoto ya elimu,miaka 19 yote ilikuwa safari yenye milima na mabonde faraja,ni moja ya safari yakusaidia na kuwainua wanafunzi waliokata tamaa katika elimu,sisi tupo kwa ajili ya kutumika ili wale wanaooonekana hawawezi wapigiwe saluti,"alisema Tabaro.

Alisema katika kipindi chote chakuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa na ufundishaji ambao ni tofauti kna watu wengine na kuwawezesha zaidi ya wanafunzi 700 kujiunga na vyuo katika ngazi shahada.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...