Na Mariam Mkamba, Tabora

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Stephen Wasira, amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii na kutumia elimu kama silaha ya kujiletea maendeleo, huku akiahidi kufikisha changamoto zao kwa wahusika ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza Aprili 16, 2025 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Dkt. Batilda iliyopo wilayani Kaliua, mkoani Tabora, Wasira alisema serikali ya CCM itaendelea kuwekeza kwenye elimu kwa lengo la kuijenga jamii imara inayojitegemea.

Hivyo basi, ameeleza kuwa changamoto ya uhaba wa walimu kwa baadhi ya masomo ni moja ya maeneo yatakayopatiwa kipaumbele, huku akiahidi kuzungumza na mamlaka husika ili kuongeza nguvu ya ufundishaji kwa wanafunzi.

“Tutashughulikia changamoto zote mlizonazo. Hii ni shule muhimu kwa ajili ya kumuinua mtoto wa kike. Lazima tuhakikishe mazingira yake yanakuwa bora,” alisema Wasira mbele ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo.

Akiendelea, Wasira alisema ujenzi wa shule hiyo ni ishara kuwa nafasi ya mwanamke katika jamii ya sasa imeimarika, akisisitiza kuwa wanawake wa sasa si wa kubaki nyuma tena bali ni sehemu ya maendeleo ya taifa.

Pia, amewashukuru wanachama wa CCM wilayani Kaliua kwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa kazi kubwa amefanyika katika kipindi kifupi cha uongozi wake ni ishara tosha ya dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania.

Akihitimisha hotuba yake, Wasira amesema kwa msisitizo: “Samia mitano tena. Kazi iendelee.”




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...