Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Stephen Wasira amesema nchi ya Tanzania inaweza kusimama kifua mbele katika miaka 61 imekaa bila kuwa na matatizo ya kijeshi,bila mapinduzi.

Amesema majeshi yetu yalikuwa hayawezi kubaguana kwa kuwa wote walijiona ni wamoja ndio maana tukaanzisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania huku akieleza kwamba hakuna jeshi duniani ambalo halifanyi siasa ya nchi yake.

Wasira amesema hayo alipokuwa akizungumza na wana CCM na wananchi wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma ambako ameanza ziara ya kikazi sambamba na kuzungumzia faida za muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanikisha kuwa na Taifa la Tanzania ambao umefikisha miaka 61 sasa.

“Wako wanasiasa wanasema ninyi mnachanganya majeshi na siasa , sisi tunawaambia ninyi hamuelewi mambo mtuulize sie tuliekuwepo tumetawala miaka.Hakuna jeshi duniani ambalo halijui siasa ya nchi yake .

“Jeshi la namna hiyo ni la kukodisha lakini jeshi la kweli linajua.Mnaliambia muendee mpigane wanasema tunapigana kwa nini?Mtu huwezi kuwa mwendawazimu utaenda kufa bila sababu…

“Lazima unasababu na sababu yenyewe unapenda nchi unayoifia na hiyo ni siasa.Hata Marekani wanaosema msiingize siasa wanafanya siasa katika majeshi yao siasa yao ni kwamba wawe Polisi wa dunia,amesema Wasira.

Ameongeza kwahiyo wanasema wao (Marekani)nchi zote zitii amri zao na ikivunjwa wanakwenda kuwapiga kwasababu ya kuwashikisha adabu ili mtii siasa ya nchi yao.

“Wanafanya siasa.Wewe unaweza kukusanya watu ukawapa bunduki bila sababu kwani wanaweza kukugeukia wanasema wewe sasa ndio zamu yako,”amesema Wasira.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...