NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KLABU Yanga imeendelea kung'ang'ania kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania bara mara baada ya kuichapa Tabora United 3-0.

Katika mchezo huo wa aina yake ambao ulipigwa katika dimba la Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora tumeshuhudia Yanga wakiutawala mchezo kuanzia filimbi ya mwanzo wa mchezo hadi dakika 90 na kufanikiwa kuondoka na ushindi huo mnono.

Israel Mwenda ndiye alianza kufungua mlango wa mabao kwa kupachika bao safi kwa mpira wa adhabu kipondi cha kwanza.

Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumuingiza kiungo mshambuliaji wao Ikangalombo akichukua nafasi ya Max Nzengeli licha ya kutengeneza nafasi nyingi za mabao lakini hakufanikiwa kuonesha makali yake.

Mzize nae kama anatafuta kiatu cha ufungaji bora ligi kuu licha ya msimu ulipita kuchukua kiatu cha ufungaji bora kombe la Shirikisho, amefanikiwa kufikia mabao 11 ndani ya ligi kuu mara baada ya leo kupachika bao moja.

Naye Prince Dube hakuwa nyuma, amepachika bao lake la 11 ndani ya ligi kuu Tanzania bara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...