Dar es Salaam, Tanzania –Mei 2025. Absa Bank Tanzania
imezindua rasmi mpango wake wa mazingira wa Blue Ocean Initiative, ukiwa
umehamasishwa na jitihada za kimataifa kama vile Blue Climate Initiative (BCI)
inayotambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa kupitia Muongo wa Sayansi ya Bahari
kwa Maendeleo Endelevu.
Uzinduzi huu umeanza kwa zoezi kubwa la usafi wa Ufukwe wa
Kawe, likihusisha wafanyakazi wa Benki 100 wa kujitolea na Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, ambao walikusanya taka na plastiki kwa kipindi cha saa 4
- na hivyo kutoa jumla ya saa 400 za kujitolea za wafanyakazi wa Benki ya Absa
kwa ajili ya afya ya bahari na ustahimilivu wa hali ya hewa.
Akizungumza katika tukio hilo, Oscar Mwamfwagasi, Afisa Mkuu
wa Uendeshaji alisema: “Kama Blue Climate Initiative, tunaamini bahari si
mwathirika tu wa mabadiliko ya tabianchi - bali pia ni sehemu muhimu ya
suluhisho. Kupitia Blue Ocean Initiative, tunachukua nafasi yetu ndani ya
harakati hizi za kimataifa, tukianza hapa nyumbani.”
Mpango huu unaakisi dhamira ya Absa kupitia madhumuni yake
ya msingi:“Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja… Stori moja baada ya nyingine.”
Aron Luhanga, Mkuu wa Masoko na Mahusiano ya Kijamii,
aliongeza: “Taka za plastiki husababisha vifo vya zaidi ya wanyama wa baharini
milioni 100 kila mwaka. Ni wakati wa mashirika kuchukua hatua madhubuti.
Kupitia mpango huu, tunadhihirisha maana ya ahadi yetu - Stori yako ina thamani
- na kuwa kichocheo cha mazuri katika jamii.”
Absa inalenga kupanua mpango huu katika fukwe nyingine za Tanzania huku ikiendelea kujenga ushirikiano wa kijamii kwa ajili ya uhifadhi endelevu wa bahari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...